Skip to content
Media

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Dr. Salim Ahmed Salim Yaadhimisha Mwaka Mmoja kwa Maudhui Mapya

  • Share

Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Dr. Salim Ahmed Salim Yaadhimisha Mwaka Mmoja kwa Maudhui Mapya

Dar es Salaam, Tanzania: Tovutiy ha Hifadhi ya Nyaraka za Dr. Salim Ahmed Salim (SAS Digital Archive) inasherehekea mwaka wake wa kwanza kwa kutoa maudhui mapya ya kipekee ambayo hayajawahi kuonekana, yakitoa mwanga kuhusu mojawapo ya wanadiplomasia wenye ushawishi mkubwa barani Afrika. Tukio hili muhimu linathibitisha zaidi dhamira ya Maktaba hii ya kutunza urithi wa Dr. Salim na kuimarisha hadhi yake kama kituo cha kimataifa cha wasomi na wapenda historia.

Maktaba hii imezindua nyaraka mpya zilizohifadhiwa kidijitali, zikiwemo maelezo binafsi kutoka kwenye mikutano muhimu na viongozi wa Afrika kama Rais Hassan Gouled Aptidon wa Djibouti, Rais Isaias Afwerki wa Eritrea, Waziri Mkuu Meles Zenawi wa Ethiopia, na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. Miongoni mwa nyaraka hizo, kuna taarifa maalum kuhusu vita vya Ethiopia na Eritrea vilivyohusisha mji wa Badme vilivyoanza Mei 1998.

Moja ya maelezo binafsi ya Dr. Salim kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea yanaonyesha changamoto kubwa za kidiplomasia alizokutana nazo wakati wa vita vya Badme. Katika tukio la kusisimua, Balozi David Shinn wa Marekani alimtafuta Dr. Salim kuomba msaada wake juu ya suala tofauti lililomhusu Jenerali Sani Abacha wa Nigeria, akimshauri asiwauwe waliopanga njama za mapinduzi. Tukio hili linaonesha hali ya changamoto za kidiplomasia ambazo Dr. Salim alikabiliana nazo:

"Itakuwa ni kosa kubwa kwa Nigeria ikiwa waliokutwa na hatia watahukumiwa kifo. Ikiwa Jenerali Abacha anatarajia kuwa Rais wa Nigeria kama watu wanavyodai, basi itakuwa ni ishara mbaya endapo hatua yake ya kwanza kama Rais wa kiraia itakuwa ni kuwauwa watu hao. Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kuwa hawauawi."

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2023, Maktaba ya Kidijitali ya SAS imevutia zaidi ya watumiaji 18,000 kutoka Marekani, Ulaya na Afrika, na kuwa rasilimali muhimu kwa wasomi na wapenda historia wanaotafiti nafasi ya Tanzania katika diplomasia ya kimataifa. Maktaba ina mpango wa kuimarisha ushirikiano wake na taasisi kama Chuo Kikuu cha Columbia na Kituo cha Salim Ahmed Salim cha Mahusiano ya Kigeni ili kukuza majadiliano kuhusu uongozi, utawala, na nafasi ya Afrika katika masuala ya kimataifa.

**MWISHO**

Soma zaidi kuhusu maudhui mapya:


Press-Release-_-Salim-Ahmed-Salim-_-October-2024_SWA.pdf

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Dr. Salim Ahmed Salim Yaadhimisha Mwaka Mmoja kwa Maudhui Mapya

Press-Release-_-Salim-Ahmed-Salim-_-October-2024_SWA.pdf
206 KB
Go to external page: Download